Windows

Mtibwa Sugar U20 yaifunga Simba U20, yatinga fainali



Mchezo wa nusu fainali ligi kuu ya vijana kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba umemalizika kwa Mtibwa Sugar kuendelea hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1

Simba ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya tano kupitia kwa Modest Matinyanga

Hata hivyo Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo, walikuja juu na kufanikiwa kurejesha bao hilo kisha kufunga mengine mawili

Mtibwa Sugar sasa itacheza na Azam Fc kwenye mchezo wa fainali

Post a Comment

0 Comments