MADRID, HISPANIA.MANCHESTER United na Real Madrid zimeripotiwa kupishana kidogo kwenye makubaliano ya kuhusu bei ya kiungo Mfaransa, Paul Pogba.
Man United imesema staa wao huyo anauzwa kwa Pauni 150 milioni na hawataki kujadili kwamba hakucheza kwa kiwango kikubwa msimu uliopita na kwa miaka mitatu tangu walipomnasa kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia wakati huo, Pauni 89 milioni kutoka Juventus.
Taarifa zinasema kwamba Real Madrid wao wana kiasi cha Pauni 135 milioni, ambayo itakuwa pungufu kwa Pauni 15 milioni kutoka kwenye dau lile la Man United wanalomuuza staa huyo.
Mkataba wa Pogba huko Old Trafford utafika tamati 2021 huku kuna makubaliano ya kuongeza mwaka mmoja, hivyo bado kuna nafasi ya kuendelea kuwa na thamani kubwa hivyo kutokana na mkataba wake bado kuwa mrefu.
Jambo hilo ndilo linalowafanya Man United kuweka ngumu wakiilazimisha Real Madrid kukubali masharti yao kama kweli wanahitaji huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Mabingwa wa Italia, Juventus nao wanahitaji saini ya mchezaji huyo, lakini Man United yenyewe imeshaweka wazi bei yake,
Pauni 150 milioni ndio watakaa mezani kuanza mazungumzo.
0 Comments