Windows

Kotei ajiweka sokoni


KIUNGO Simba, James Kotei raia wa Ghana hajasaini mkataba mpya na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na baada ya kuona mabosi wake wamekaa kimya ameamua kujiweka sokoni.

Kotei ambaye aliibuka kiungo bora katika tuzo za Mo Simba Awards yupo kwao baada ya ligi kumalizika ambapo aliondoka nchini pasipo kufanya mazungumzo mapya na mabingwa hao ingawa kuna taarifa kwamba wana mpango wa kumtema.

Kuna taarifa kwamba timu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini inahitaji huduma ya kiungo huyo ingawa hajaweka wazi juu ya hilo na kwamba timu yoyote atakayopata ataitumikia ikiwemo kurudi Simba kama atahitajika.

“Mkataba wangu wa miaka miwili wa kuutumikia Simba umemalizika na mpaka sasa sijasaini timu yoyote ila wakala wangu yupo katika mazungumzo na timu nyingi za nchi mbalimbali, timu atakayokubaliana nayo basi nitakwenda huko.

“Chaguo langu la kwanza ni Simba kuendelea kubaki hapo lakini ikishindikana kutokana na sababu za kushindwa kukubaliana nitakuwa sina namna nyingine zaidi ya kuachana nao, muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi, Simba nimekaa nao vizuri ndio maana naipa nafasi ya kwanza," alisema Kotei.

Post a Comment

0 Comments