Windows

Maandalizi ya KUBWA KULIKO usipime



Yanga imedhamiria kuandika historia Jumamosi hii inayokuja katika tukio kubwa la Harambee ya kuichangia timu hiyo

Tiketi zimeendelea kuuzwa kupitia mitandao ya simu Tigopesa na Mpesa ambapo kuanzia kesho Jumanne tiketi zitaanza kupatikana maeneo mbalimbali

Mapema leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga Anthony Mavunde na wajumbe wa kamati hiyo Richard Kalongola na Pelegrinius Rutayuga walifika studio za Azam TV kuweka sawa taratibu za urushwaji wa matangazo 'mbashara' kupitia kisimbuzi cha Azam

Kesho Mavunde pamoja na timu yake, kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya Yanga, watazungumza na waandishi wa Habari kutoa taarifa ya maandalizi ya tukio hilo la kihistoria

Kwa wale ambao hawana tiketi, wameaswa kujipatia tiketi mapema ili kuwa sehemu ya historia itakayoandikwa Jumamosi, Juni 15 2019

Post a Comment

0 Comments