

Leo uongozi wa Simba umethibitisha kumpa mkataba wa miaka miwili nahodha wake John Bocco
Taarifa ya Bocco kusaini mkataba wa miaka miwili imetolewa mapema leo
Hata hivyo Bocco alisaini mkataba huo kabla hajatimkia Misri
Sio Bocco pekee, hata nyota wengine wa Simba ambao wako na timu ya Taifa huko Misri nao walisaini
Aishi Manula, Erasto Nyoni na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' nao wameshamalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Kinachosubiriwa ni taarifa rasmi kutolewa na uongozi wa Simba
Usajili wa Simba umekuwa ukifanywa kwa usiri mkubwa hali inayopelekea hofu miongoni mwa mashabiki wake ambao wamezoea 'vurugu' za wekundu hao wa Msimbazi kwenye dirisha la usajili
Hata hivyo viongozi wa timu hiyo wamewahakikishia Wanamsimbazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa, mipango yote ya usajili itakamilishwa kama ilivyopangwa



0 Comments