

Mshambuliaji wa Mwadui Fc Salum Aiyee juzi aliisaidia timu yake kubaki ligi kuu baada ya kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold
Aiyee aliyemaliza katika nafasi ya pili katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 18, ni miongoni mwa washambuliaji walioonyesha ubora sana msimu uliomalizika
Ni bahati mbaya tu Aiyee hakupata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa lakini naamini mabao 20 aliyofunga msimu uliomalizika hakubahatisha
Ingawa Yanga haijaonyesha nia ya kumuwania mshambuliaji huyo, lakini wadau wanaamini ni miongoni mwa washambuliaji wa ndani wanaoweza kuongeza kitu katika kikosi cha Yanga
Aiyee amejiweka sokoni, yuko tayari kujiunga na timu watakayofikia nayo makubaliano
"Mkataba wangu na Mwadui umeisha, mpaka sasa nimepokea ofa nyingi zingine zinatoka nje ya nchi, bado sijafanya uamuzi nitaenda wapi au nitabaki hapahapa, sehemu nitakayokubaliana nayo ndio nitajiunga nayo " amesema Aiyee.



0 Comments