Katika toleo lililopita tuliangalia namna Kichuya alivyocheza soka la kutisha na kupata mafanikio yakiwamo yale ya kuitungua Yanga ambao ni wapinzani wakubwa wa Simba aliyokuwa akiichezea kabla ya kutimkia Misri kucheza soka la kulipwa.
Hata hivyo, kichua mafanikio hayakuishia uwanjani tu kwani mpaka sasa ana mafanikiwa makubwa nje ya uwanja. Endelea...
MALI ZAKE
Shiza ni kijana mwenye umri mdogo lakini akili yake ameiongeza kwani anawaza mambo ya maendeleo ambapo kwa kipindi alichocheza soka hasa alipohamia Simba amenunua nyumba moja ambayo ipo Mkundi, Kihonda na anaishi mtoto wa mama yake mdogo na hata yeye akienda Morogoro hufikia huko.
Nyumba nyingine anaendelea kuijenga huko Mafisa, Morogoro ila bado haijamlizika, anamiliki gari na biashara nyingine kama kusambaza chakula kwenye sherehe na shughuli mbalimbali. “Siku zote nilikuwa namsisitizia kuwekeza kwenye ardhi, nashukuru amekuwa akisikiliza maana mpira una muda wake, akistaafu bila kuwa na nyumba itakuwa ni tabu kwake, ana nyumba mbili, hapa na shamba la mpunga huko Mvomero,” anasema Mzee Mangwende
AMEKABIDHI CHUMBA
Mzee Mangwende anasema hivi sasa Shiza akienda Morogoro basi huwa anakwenda kwake kumsalimia tu lakini kulala analala kwenye nyumba yake huko Mkundi, ambapo hata chumba chake amewaachia wadogo zake wengine wanaoishi hapo.
“Nina wajukuu wengi ambao sasa wanakaa kwenye chumba alichokuwa analala Shiza, Shiza akija Morogoro lazima afike nyumbani kunisalimia na kuona nini kinahitajika,”
WATOTO WAWILI
Achana na umri wake, lakini Shiza ana watoto wawili wa kike na kiume kwa mama tofauti, Mzee Mangwende na Mzee Kichuya wana habari juu ya wajukuu hao.
Mzee Mangwende anasema: “Natamani kuwaona watoto wa Shiza, nasikia ana watoto wawili wa kike ila kwa mama tofauti, nilipewa taarifa na mjomba yake ambaye ni mwanangu anaitwa Issah kuwa huku kuna wajukuu, nadhani wote anawahudumia ingawa huyu mwanamke wake wa pili tulionana na familia yake kwani kuna mambo tulienda kuyatatua.
“Nitafurahi siku moja Shiza kama siyo kuniletea watoto wake niwaone basi anipeleke nikawaone mwenyewe hivyo nasubiri maamuzi yake tu, maana hiyo ni damu yetu,”
“Yule mwanamke wa kwanza nasikia aliwahi kumpigia simu hata bibi yake Shiza, alimtumia Sh 30,000 ila sijawahi kumuona. Huyu mwingine alikuwa anaikataa mimba ila ikabidi hadi waende kupima na ikagundulika kama kweli ni mwanaye, hivyo ilifanyika jitihada ya kuonana na baba yake mdogo na yule binti na mimi mwenyewe. Ila sasa hivi nadhani anamhudumia na aliniambia atajua jinsi ya kuhudumia, siku hizi sipati malalamiko yoyote.”
JINA LA SHIZA
Mzee Mangwende anasema jina Shiza kwa mila zao humpa mtoto aliyezaliwa kwa kuwafuata watoto pacha ambapo Shiza yeye alitanguliwa na kaka zake mapacha.
ANALICHUKIA JINA LA KICHUYA
Anaeleza kuwa kutokana na umaarufu wa mjukuu wake hasa akijulikana kwa jina la Kichuya basi hata yeye wakati mwingine huitwa jina hilo ambalo halitaki kwani ni jina la baba yake Shiza.
“Kiukweli umaarufu wa Shiza unanifanya hata mimi wakati mwingine waniite Mzee Kichuya jina ambalo siyo langu, nakasirika bora hata mtu mwingine tungekuwa na mahusiano mazuri,” anaeleza.
BABU AMPA MBINU
“Nilimwambia mpira una muda, ajifanyie kitu cha maisha yake kwanza, anaweza kuumia ama lolote likatokea halafu akashindwa kucheza, wapo waliotumia vizuri vipaji vyao walinunua nyumba mpira ulipoisha wanaingiza pesa kutumia kodi ya nyumba zao,” anasema Mzee Mangwende.
NIDHAMU
Anasema kwenye nidhamu yake aliwahi kumweleza kuwa aheshimu kila mtu; “Alipotoka Mtibwa alikuwa anafunga sana karibu na mabao kama 12 hivi, sasa hivi hafungi hata mpira huwa hawampi pasi, tangu alipowafunga Yanga hajafunga tena.
“Wakati mwingine wanamuweka benchi, ama anacheza kidogo anatolewa, nilimwambia ajiangalie wenzake walikuwa wanamzunguka, kuna mawili inawezekana utovu wa nidhamu ndiyo maana waliona wamuuze tu Misri.
“Hata alivyokuja timu ya Taifa napo hakupangwa, nasikia hata sasa ameitwa hivyo anatakiwa kujiangalia zaidi wapi amekosea, mpira una muda mfupi, ajiwekee akiba kwa ajili ya mpira utakapoisha,”
“Alipokuwa hapa nilijua tabia zake zote ila kwa vile anaishi huko sijui mabadiliko yake ya kinidhamu, kama ana utovu wa nidhamu anaweza kupotea mapema, kama anafanya starehe basi nazo zitampoteza, maana hapa hakuwa mtu wa starehe kama kunywa pombe, uvutaji sigara na kama ameanza kufanya hayo mambo aache mara moja,” anasema Mzee Mangwande
MZEE KICHUYA ATOA NENO
Mzee Kichuya yeye hakutaka kuzungumza mambo mengi juu ya mwanaye; “Kama nilivyosema hapo awali kuwa haya mambo tumuachie Mungu kwani ndiye anayejua ukweli kwamba mimi nimehusikaje kwa Shiza, unajua sisi ni binadamu muda mwingine tunapaswa kuacha mambo mengine yapite tu.
“Kikubwa ninachomtaka mwanangu ni kuwa na nidhamu, kuheshimu kila mtu maana huwezi kujua kesho yako, apambane kadri ya uwezo wake, asifanye starehe zisizokuwa na maana ambazo zitamrudisha nyuma.
“Nafahamu kama ana watoto wawili, nimeambiwa, basi awalee katika maadili mema, naamini ipo siku tutakaa na kujadili mambo ya maendeleo zaidi ila hapa alipofika hata kujenga nyumba ni moja ya hatua kubwa kwake, hajab weteka na wala hajajisahau.
“Kiukweli huwa tunawasiliana vizuri tu, kabla hajaenda Misri hata kwangu alikuwa anakuja na msaada alinipatia. Mimi ni shabiki wa Yanga na kipindi alichokuwa anatufunga basi alikuwa anakuja Morogoro kunipa pole ananiachia pesa.”

0 Comments