Waziri wa mambo ya nje wa Morocco juzi alitangaza kuwa, kamati ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika itafanya mkutano leo mjini Skhirat.
Mkutano huo wa siku tatu utakagua hatua za ujenzi wa amani barani Afrika, njia ya kufanya kazi ya kamati hiyo na changamoto za kutatua mgogoro barani Afrika.
Mkutano huo utahudhuriwa na nchi wanachama 15 wa kamati hiyo, zikiwemo Algeria, Angola, Burundi, Djibouti, Gabon, Guinea Ikweta, Kenya, Lesotho, Liberia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, Togo, Zimbabwe na Morocco.
0 Comments