Windows

Juma Kaseja Asani Miaka KMC Leo

KIPA wa KMC, Juma Kaseja leo Jumamosi Juni 22, 2019 ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu yake ya KMC aliyoichezea msimu uliopita.

 

Akiwa na kikosi hicho Kaseja amewapa changamoto makipa wenzake, Jonathan Nahimana pamoja na Dennis Richard hali iliyofanya kikosi hicho kuwa imara.

 

Kipa huyo ameiongoza KMC akiwa Nahodha ambapo walimaliza ligi wakishika nafasi ya nne kutokana na mwenendo mzuri ikiwa chini ya kocha Ettien Ndayiragije ambaye sasa ni kocha wa Azam FC.

 

Wachezaji wengine walioongezwa mikataba KMC ni Charles Ilanfya, Dennis Richard, Rehan Kibingu, Sadala Lipangile, Cliff Buyoya, Ismail Gambo, Omary Ramadhan, Abdul Hillary, Ally Ramadhan na Rayman Mgungila.

The post Juma Kaseja Asani Miaka KMC Leo appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments