

HII sasa wanayofanya Yanga ni sifa maana kila Jembe wanalipa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu Mwinyi Zahera.Mpaka sasa tayari mashine 9 tayari zimemalizana na Yanga huku mmoja tu Papy Tshishimbi akiongezewa mkataba wa miaka miwili.
Usajili wa jana wa beki kiraka kutoka KMC ambaye alipokelewa na mashabiki wa kutosha pale Jangwani tayari anafanya jumla ya wachezaji 10 wawe wamemwaga wino ndani ya Yanga mpaka sasa.
Hivyo Ally maarufu kama mwarabu anaungana na wachezaji wenzake ambao ni pamoja na :Patrick Sibomana wa Rwanda, Lamine Moro wa Ghana, Issa Bigirimana wa Rwanda, Maybin Kalego wa Zambia.
Mustapha Suleiman wa Burundi,Juma Balinyi wa Uganda, Sadney Urikhob wa Namibia, Abdulaziz Makame ametoka visiwani Zanzibar
na Papy Tshishimbi ameongeza mkataba wa miaka miwili yeye anatokea Congo.



0 Comments