WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Misri, waeanza kampeni yao ya kuwania taji hilio kwa kuilaza Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa mjini Cairo usiku wa kuamkia leo.
Mahmoud Trezeguet alifunga bao la kipekee la mchezo huo kabla ya muda wa mapumziko.
Mashambuliaji wa Liverpool, Mo Salah, alikaribia kutia kimiani bao la pili katika kipindi cha pili lakini kipa wa Zimbabwe Edmore Sibanda hakumpatia nafasi.
Ovidy Karuru aliipotezea Zimbabwe nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo la Misri katika mashambulizi ya dakika za mwisho.
Mashindano ya mwaka huu ya Afcon ambayo yanajumuisha timu 24 ndiyo makubwa zaidi kuchezwa msimu wa joto.
Sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo ilisheheni mbwembwe za kila aina huku mashabiki 75,000 wakijitokeza kuishangilia timu yao ya nyumbani katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Lakini mchezo wenyewe haukufikia kiwango cha msisimko wa sherehe ya kuvutia ya ufunguzi baada ya Misri kutawala mchezo huo bila kumfikia kipa Sibanda wa Zimbabwe kama ilivyotarajiwa.
Salah aliongeza nakshi mchezo huo kwa kufanya mashambulizi mara kadhaa katika kipindi cha kwanza japo hakupata fursa ya kufunga bao moja kwani kipa Sibanda alikuwa macho.
Zimbabwe walianza kufurahia mkondo wa mchezo kabla ya Misri kuchukua uongozi katika kipindi cha kwanza.
Ushirikiano mzuri wa Trezeguet na wachezaji wenzake uliiwezesha Misri kufika karibu na lango la Zimbabwe lakini washambuliaji wa Misri kila mara walishindwa kupenya ngome ya wapinzani wao.
Mo Salaha alijitahidi kupata bao lakini juhudi zake zilizimwa na kipa wa ziada wa Zimbabwe, Elvis Chipezeze, ambaye aliingia uwanjani baada ya Sibanda kujeruhiwa dakika 10 za mwisho wa mchezo huo.
Ushindi huo wa Misri umeiweka katika nafasi ya kwanza ya kundi A ambayo pia inajumuisha DR Congo na Uganda. ambao watamenyana leo Jumamosi katika uwanja huohuo.
The post AFCON 2019: Misri Waichapa Zimbabwe 1-0, Mechi Ya Uzinduzi appeared first on Global Publishers.
0 Comments