Windows

Yanga yatenga Bilioni Mbili kwa ajili ya usajili


Uongozi wa Yanga umetenga kati ya Tsh Bilioni 1.5 hadi Bilioni mbili kwa ajili ya usajili wa msimu ujao
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Lucas Mashauri amesema walikutana na kocha Mwinyi Zahera ambapo aliwapa mchanganuo wa mahitaji yake kwa ajili ya usajili
"Bajeti ya usajili mara nyingi inatolewa baada ya kukamisha zoezi la usajili"
"Lakini kwa sasa tunakuwa na makisio ya Bajeti tunayohitaji ambapo Kamati yetu ilipewa kazi ya kutafuta kati Bilioni 1.5 na Bilioni mbili," amesema
"lengo letu kubwa ni kuwa na Yanga imara msimu ujao. Kazi tumemuachia kocha Mwinyi Zahera ili atuambie wachezaji anaowahitaji"
"Bajeti halisi itafahamika baada ya kocha kujadiliana na wachezaji anaotaka waje"
"Lakini tumemuhakikishia, hakuna mchezaji ambaye atamuhitaji tutashindwa kumsajili. Awe Tanzania, nje ya Tanzania hata Ulaya akipatikana mchezaji tutamsajili. Yanga imeshawahi kusajili wachezaji kutoka Ulaya"
"Kamati yetu inaendelea na zoezi la kutafuta fedha ili tuweze kutimiza lengo la kusajili timu bora kadiri kocha atavyopendekeza"
Katika hatua nyingine, Mashauri amewataka Wanayanga waendelee kuichangia timu yao waepuke upotoshaji unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
"Tunawataka wapenzi, wanachama na mashabiki wetu waendelee kuichangia timu wasipotoshwe na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao"
"Taarifa nyingi zinazosambazwa kuwa tumepokea Bilioni mbili hazina ukweli wowote. Wanaoanzisha taarifa hizo wana lengo la kupunguza kasi ya kuichangia timu yetu"
"Yanga ni timu ya Wananchi na safari hii tumeamua kuisimamia sisi wenyewe. Na kama alivyosema Mwenyekiti, zoezi hili la uchangiaji litandelea kwa kuwa ni wajibu kwa kila Mwanchama wa Yanga kuichangia timu kila mwezi Tsh 1000/- ambayo ni ada ya uanachama"

Post a Comment

0 Comments