

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema malengo yao msimu huu hayakuwa kushiriki michuano ya kimataifa na hata kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Kauli hii imekuja mara baada ya kipigo cha jana dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Kombe la FA
Zahera amedai hata kwenye ligi malengo yao hayakuwa kubeba ubingwa lakini baada ya kuwa wanacheza na wanashinda wakaamini kuwa wanaweza kubeba ubingwa.
Zahera ameongeza kuwa hawana cha kupoteza kipindi hiki na sasa wanajipanga kwa msimu ujao baada ya kushindwa kuwa mabingwa wa kombe na ASFC.
Na kuhusu Ligi Kuu, Zahera amesema wana nafasi dogo sana ya kuwa mabingwa kutokana na klabu ya Simba kubakiza mechi nyingi zaidi yao.




0 Comments