

Baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Kombe la FA, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema walikuwa na malengo ya kumaliza ligi katika nafasi ya tano au sita.
Kauli ya Zahera imekuja mara baada ya kuona ndoto hizo zinaenda mkono wa kushoto kulingana na namna mwenendo wa ligi ulivyo hivi sasa.
Zahera amefunguka hayo akiwa amepoteza malengo mawili mpaka sasa ikiwemo taji la SportPesa na Kombe la Shirikisho ambayo aliahidi kuwa wanaweza wakachukua.
Mbali na mataji hayo, Zahera pia aliahidi kutwaa taji la ligi lakini kwa namna msimamo ulivyo hivi sasa katika Ligi Kuu Bara uhakika wa kutwaa taji hilo haupo kutokana na watani zao wa jadi Simba kuwa vizuri zaidi.
Baada ya kupoteza mchezo wa jana, kikosi cha Yanga kinatarajia kusafiri kuelekea Mara kwa ajili ya mechi na Biashara United ambayo ni ya ligi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Karume.




0 Comments