


Unakumbuka kipindi kile Afisa habari wa Yanga Dismas Ten alipokuwa akipost picha za mchezaji wa Simba Said Ndemla mara kadhaa akipost bila maelezo na mara nyingine akitoa maelezo (Caption) ambazo siyo rahisi kuelewa nini alikuwa anamaanisha?
Basi Taarifa ikufikie msomaji wa Kwata Unit tu kuwa inaelezwa kuwa Yanga imeshafanya mazungumzo na Said Ndemla na wamekubaliana kila kitu kuhusu kutua Jangwani.
Licha ya mchezaji Said Ndemla kuwa na uwezo mkubwa sana uwanjani lakini amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kocha Patrick Aussems kiasi cha kuelezwa kuwa amekuwa hana furaha na amekuwa akitaka kupata klabu ambayo atapata nafasi ya kucheza.
Katika dili hilo jipya inaelezwa kuwa Said Ndemla atasaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Yanga.



0 Comments