Windows

Simba wafunguka kama kweli wamemalizana na Ajibu

Wakati kukiwa na fununu kuwa mchezaji wa Yanga wa sasa Ibrahim Ajibu kuwa amewatema Tp Mazembe ili tu kujiunga na Simba , Simba wenyewe wamekuja na tamko lao la kuthibitisha kama ni kweli au si kweli.


Awali ilielezwa na kuthibitika kuwa Ibrahim AJibu anahitajika na Tp Mazembe na Hata kocha wa Yanga Zahera Mwinyi alithibitisha juu ya Taarifa hiyo.

Siku kadhaa zilizofuata Tp Mazembe wakatangaza kushindwana na Ajibu kwenye baadhi ya vipengele huku ikielezwa Simba kuhusika kwenye dili hilo la kusababisha mpaka Ajibu ashindwe kujiunga na Mamba hao wa Lubumbashi.
Afisa habari wa Simba Haji Manara msomaji wa Kwata Unit amefunguka kuwa taarifa za wao kumalizana na Ibrahim Ajibu hazipo kama ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikisema.

” Hatujaanza mazungumzo naye hizo ni taarifa ambazo zinasemwa tu mitandaoni, Taarifa rasmi ya klabu kuhusu usajili itatolewa wakati sahihi ukifika “

Post a Comment

0 Comments