

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi chake kipo fiti kuivaa Lipuli ya Seleman Matola anaamini atashinda mchezo wake wa Jumatatu ikiwa ni hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho.
Zahera amesema kuwa anatambua kwamba Lipuli ni wazuri wakiwa nyumbani licha ya kuwafunga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uwanja wa Samora wasitarajie watafanikiwa tena.
"Sikuepo wakati timu ya Lipuli inaifunga Yanga, ila nilikuja kuangalia ripoti na matokeo nikagundua kwamba, wapinzani wetu walibahatisha kwani walipiga shuti moja kwenye lango na wakatufunga bao moja.
"Sasa nikawaambia vijana wangu mmecheza vizuri, msiwe na mashaka huu ni mpira tukikutana nao wakati mwingine lazima tushinde, hivyo tutaingia kwa mbinu mpya kutafuta matokeo," amesema Zahera.
Mshindi wa mchezo wa jumatatu, atakutana na Azam FC ambao walishinda jana kwa bao 1-0 mbele ya KMC.



0 Comments