Windows

YANGA; HAYA YAKIFANYIKA TUTAKUWA NA LIGI BORA BONGO


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ili Tanzania kuwe na maendeleo ya soka inapaswa waamuzi wafuate sheria 17 za mpira pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania kutoa adhabu kwa wakati kwa wale wanaokiuka utaratibu.

Zahera amekiongoza kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa ambapo mpaka sasa kipo nafasi ya pili kikiwa kimejikusanyia pointi 80 baada ya kucheza michezo 35.

Zahera amesema kuna mambo mengi ambayo yanatokea kwenye soka yanawaumiza wachezaji pamoja na viongozi wa timu hivyo ili kuleta maendeleo yapaswa kuyafanyia kazi.

"Kuna mambo mengi ambayo yanaendelea hapa kwenye ligi, nadhani kama waamuzi watakuwa wakichukuliwa hatua baada ya kukiuka sheria italeta msaada hapo baadaye kwani wengi watakuwa makini na kuifanya ligi kuwa na ushindani.

"Pia wahusika wenyewe wakijali na kufuatilia haya ambayo yanatokea kwenye ligi tutakuza mpira,ila kama hakuna anayejali basi tutabaki kurudi nyuma na kuishia kuwa wasindikizaji kwenye mashindano ya kimataifa," amesema Zahera.

Post a Comment

0 Comments