EMMANUEL Okwi mshambuliaji wa Simba mwenye mabao 14 kwa sasa amesema kuwa alipoteza dira ndani ya Simba kwa kukata tamaa ya kurejea kwenye ubora wake ndani ya kikosi hicho kutokana na kushindwa kufunga mabao kwa muda mrefu ila anawashukuru wachezaji wa Simba na benchi la ufundi kumpa moyo.
Okwi msimu uliopita wa mwaka 2017/18 aliibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao 20 msimu huu alianza kwa kusuasua kabla ya kureja kwenye ubora wake baada ya kikosi hicho kuanza ziara za kanda ya ziwa.
"Sikuwa kwenye wakati mzuri nyuma, ila nashukuru Mungu wachezaji wenzangu walinipa moyo na kunifanya niamini kwamba ninaweza kurejea kwenye ubora wangu kwa sasa nimeanza kuwa katika ramani hilo ni jambo la kushukuru.
"Bado tunaendelea kupambana mashabiki watupe sapoti kwani kazi yetu iliyo mbele ni kubwa na kila mmoja anatafuta matokeo chanya, nina imani tutafanya vizuri," amesema Okwi.
0 Comments