KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wakati wa lala salama timu nyingi zinapambana kutafuta matokeo hata kwa njia ambazo si halali hivyo ni wajibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatilia kila hatua nyakati hizi.
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kukamilika Mei 28 ambapo ndipo itajulikana ni nani atashuka daraja baada ya African Lyon kutangulia kuporomoka msimu huu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kila timu kwa sasa inahaha kutafuta matokeo ili kuona ni namna gani itabaki kwenye ligi.
"Kwa sasa ligi ipo kwenye lala salama ni wakati muafaka wa kutazama namna inavyokwenda hasa kwa TFF ambao ndio wasimamizi, nyakati hizi wengi wamekuwa wakitumia mbinu za ovyo kutafuta matokeo.
"Timu ambazo zimepanda Daraja ambazo ni Namungo ya Lindi pamoja na Arusha United ya Kilimanjaro ni muda wa kuanza kujipanga kwani huku kuna mambo mengi ambayo yanatokea hasa lala salama, isije ikawa zimepanda na kuishia kushiriki," amesema Matola.
0 Comments