

Makonda kuwapa fedha walioshinda tuzo
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ameahidi kuwapa fedha Tsh Milioni Moja wachezaji wote walioshinda tuzo leo katika hafla ya Mo Simba Awarda iliyofanyika Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam leo
Aidha Makonda ameahidi kumpa Tsh Milioni 10, mlinda lango Aishi Manula
Nitarudi Simba - Samatta
Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mbwana Samatta amesema akistaafu soka la Kimataifa na kurejea nchini, timu ambayo atapenda aitumikie kabla ya kutundika 'daluga' ni Simba
Samatta leo alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa kwenye hafla ya utolewaji wa tuzo kwa wachezaji na wadau wa klabu ya Simba
"Nilikuwa mchezaji wa Simba zamani, hata nitakaporudi baadaye nafikiri nafasi ya kwanza itakuwa kwa Simba kwa sababu niliwahi kuitumikia lakini kama watakuwa hawanitaki ndio nitaangalia sehemu nyingine," amesema Samatta
"Kwa heshima yao kwa sababu niliwahi kuwa mchezaji wao kwa hiyo nafasi ya kwanza lazima itakuwa kwao"
Mo awataka wachezaji watambue ukubwa wa Simba
Mwekezaji wa Simba Sc Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, amewataka amewataka wachezaji na benchi la ufundi watambue thamani ya klabu hiyo
Akizungumza kwenye hafla ya utolewaji tuzo kwa wachezaji wa Simba, Mo alisema jana mashabiki wa timu hiyo waliwaonyesha ukubwa wa klabu wanayoitumikia walipojitokeza kwa wingi kuwapokea baada ya kutwaa ubingwa
"Naomba niwaambie Simba ni timu kubwa Tanzania na timu kubwa Afrika , mliona jana Dar es salaam ilivyoochafuka wakati tulipoleta kombe la Ubingwa, wachezaji na benchi la ufundi mtambue thamani ya simba kuna watu wanaumia kwaajili ya simba wanaipenda," alisema Mo
Viongozi fanyeni usajili wa nguvu - Ndugai
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapa neno viongozi wote wa Simba katika kipindi hiki cha usajili.
Ndugai mgeni rasmi wa tukio hili aliwambia viongozi wa Simba wanatakiwa kufanya usajili wenye Nguvu katika kipindi hiki.
"Simba walipofiki msimu huu katika mashindano ya kimataifa wametubeba Tanzania na ili kufanya vizuri zaidi wanatakiw kufanya usajili wa maana," alisema Ndugai.
"Tumeona mapungufu mengi haswa katika michezo ya kimataifa ambayo tulifungwa mabao mengi msimu huu viongozi inatakiwa kuweka umakini na akili katika kupata wachezaji wapya wa maana," alisema.
"Naimani tukifanya usajili mzuri tutaweza kufika mbali zaidi ya msimu huu kwahiyo viongozi wote mnatakuwa kuongeza wapya waana"
Walioshinda tuzo
1. Kipa Bora wa Mwaka : Aishi Manula
2. Beki Bora wa Mwaka : Erasto Nyoni
3. Kiungo Bora wa Mwaka : James Kotei
4. Mshambuliaji Bora wa Mwaka : John Bocco
5. Mchezaji Bora Mdogo : Rashid Juma
6. Mchezaji Bora Mwanamke : Mwanahamisi Omary
7. Tuzo ya Wachezaji : Erasto Nyoni
8. Mfungaji Bora wa Mwaka : Meddie Kagere
9. Tuzo ya Heshima : Azim Dewji
10. Goli Bora la Mwaka : Clatous Chama
11. Mchezaji Bora wa Mwaka : Meddie Kagere



0 Comments