

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amesema Bodi yake bado haijakaa kujadili ripoti ya usajili iliyowasilishwa na kocha Patrick Aussems hivyo hakuna ukweli wowote juu usajiliwa kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib
Mo amesema bado hawajaanza michakato ya usajili kwa wachezaji wapya na pia wa zamani, zoezi hilo watalianza wiki ijayo
"Bado kama uongozi hatujakaa kuanza kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi na hadi sasa hakuna mchezaji yeyote ambaye tumemsajili wala kumalizana naye lakini baada ya wiki moja nitakuwa na jibu kama atakuja au la baada ya kukutana na wenzangu," amesema MO
Kumekuwa na taarifa zinazo-kinzana kuhusu kiungo huyo aliyemaliza mkataba katika klabu ya Yanga
Ajib ni zao la Simba kwani alilelewa katika timu ya vijana kabla ya kutimkia Yanga miaka miwili iliyopita
Inaelezwa alikataa kujiunga na TP Mazembe iliyokuwa ikimuwania ili aweze kujiunga na Simba, mabingwa wa Tanzania Bara



0 Comments