

Mkataba wa mshambuliaji wa Simba Emmenuel Okwi utajadiliwa baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON 2019 inayoanza Juni 21 nchini Misri, imefahamika
Okwi anatarajiwa kuitumikia Uganda Cranes kwenye michuano hiyo ambayo Afrika Mashariki itawakilishwa na timu za Tanzania, Uganda na Kenya
Okwi na Juuko Murshidi wote kutoka Simba wamejumuishwa kwenye kikosi cha Uganda Cranes
Inaelezwa Okwi anayedaiwa kuwa na ofa nyingi mkononi, ameomba asisaini mkataba sasa mpaka michuano hiyo itakapomalizika
Mwenyekiti wa Simba Swedi Nkwabi amesema anaamini Okwi atasaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga na wekundu hao wa Msimbazicut
Mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mtandao wa Inastagram, Okwi aliweka ujumbe ulioibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Simba wengi wakiamini alikuwa akiwaaga
Hata hivyo mwenyewe alifafanua kuwa ujumbe huo uliosomeka "Kwa heri ndio neno la huzuni zaidi", aliutoa katika moja ya wimbo anaoupenda sana



0 Comments