Windows

Wawa atamani kubaki Msimbazi



BEKI wa Simba, Paschal Wawa, amesema mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini bado anaipa nafasi ya kwanza timu yake hiyo kabla ya kuzifikiria nyingine ambazo zitaonyesha nia ya kumhitaji kwa msimu ujao.

Wawa aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja, amekuwa miongoni mwa mabeki waliosaidia kuifikisha timu hiyo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na BINGWA hivi karibuni, Wawa, alisema anafurahi kushuhudia akimaliza mkataba wake huku timu yake ikipata mafanikio.

Alisema endapo mabosi wa timu yake hiyo wakionyesha nia ya kuhitaji huduma yake basi hatakuwa na pingamizi lolote. “Kuna timu za ndani na hata nje ambazo zinanihiji lakini kama Simba itanihitaji lazima niwape kipaumbele kwa sababu ni timu yangu,” alisema Wawa.

Post a Comment

0 Comments