


MCHEZAJI wa timu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, amewataka vijana wanaoshiriki Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (Umisseta) Mkoa wa Dar es Salaam, kuwa na nidhamu ili waweze kufanikiwa.
Msuva aliyazungumza hayo jana wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Alisema jambo kubwa wanalotakiwa kufanya katika michezo ili waweze kufanikiwa ni kuwa na nidhamu, kuwaheshimu wazazi, walimu na wadogo zao.
Aidha, winga huyo wa zamani wa Yanga aliwataka wanafunzi hao kuwa na bidii katika masomo yao kwa kuwa michezo inaenda sambamba na elimu.
“Suala la elimu nalo ni muhimu sana, ukiwa mwanamichezo mwenye elimu utafika mbali zaidi,” aliongeza Msuva.
Michezo hiyo imeshirikisha wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Ilala.



0 Comments