Windows

Wakali wa Azam FC warudi, kuwavaa KMC

Wachezaji wa Azam FC, beki na nahodha Aggrey Morris, kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' na mabeki Mzimbabwe Bruce Kangwa na Mghana Yakubu Mohammed wanarudi uwanjani na wanatarajiwa kuanza katika mchezo wao wa leo Alhamisi saa 1: 00 usiku dhidi ya KMC, utakaopigwa Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao walikuwa nje kutokana na kila mmoja akitumikia adhabu ya kadi tatu za manjano.
Benchi la ufundi chini ya Kocha Meja Abdul Mingange amesema, wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo wakiwa na lengo la kushinda mechi zote nne walizobakiwa nazo kwenye Ligi Kuu.
"Tumejiandaa na si kwa mechi hizo za Ligi Kuu tu ispokuwa kwa mashindano yote hasa mchezo wa fainali wa FA ambao tutacheza na Lipuli FC,"alisema Mingange.
Azam inarudi uwanjani baada ya kumaliza sare ya 1-1 na Stand United ugenini.
Huu ni mchezo wa marudiano baada ya kumaliza sare ya 2-2 mechi ya mzunguko wa kwanza ya Ligi Kuu Bara mabao yakifungwa na Wazimbabwe Donaldo Ngoma na Tafadzwa Kutinyu. Pia, ni mchezo wa tatu msimu huu baada ya kukutana kwenye FA na kuwapiga bao 1-0.
Pia, itakuwa ni mara ya tatu kukutana kwenye mashindano yote msimu huu, mchezo mwingine ukiwa ni wa nusu fainali ya Kombe la FA, Azam FC ilipotinga fainali kwa kuichapa KMC bao 1-0, lililowekwa kimiani na Ngoma akiunganisha pasi ya beki wa kulia Nickolas Wadada raia wa Uganda.

Post a Comment

0 Comments