Windows

Mahakama yaagiza upande wa mashtaka kuleta majibu ya uhakika kesi ya Wambura

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura kuwa tarehe ijayo wahakikishe wanakuja na majibu yenye uhakika.
Wambura anakabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh100 milioni katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina alisema hayo baada ya Wakili wa Takukuru,Pendo Temu kudai kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.
Mhina alisema shauri hilo litakapokuja mahakamani hapo upande wa mashtaka wahakikishe wanapokuja siku ya shauri hilo waje na majibu yeye uhakika.
"Tarehe ijayo mnapokuja hapa muhakikishe mnakuja na majibu yenye uhakika,"alisema Mhina.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 23,2019 na mtuhumiwa amerudishwa rumande.
Katika kesi ya msingi mshtakiwa anakabiliwa na  mashtaka 17; shtaka moja ni la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo; mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha haramu.
Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wambura anadai, kati ya Agosti 15 na Oktoba 21, 2014, makao makuu ya Shirikisho hilo, alijipatia Sh25 milioni kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.
Pia, shtaka jingine utakatishaji fedha haramu, Mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 2015, alijipatia Sh 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali na zimetokana na shtaka la kughushi.

Post a Comment

0 Comments