Windows

Waamuzi Bara wazidi kuzongwa


LICHA ya kukubali uwezo mkubwa wa kikosi cha Simba pamoja na kipigo walichopata katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa juzi, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo amesema waamuzi ni tatizo Ligi Kuu Bara.


Mbeya City ikiwa uwanja wake wa nyumbani licha ya kuielemea Simba kipindi cha kwanza na kuongoza kwa bao 1-0, Wekundu wa Msimbazi hao walitokea nyuma kipindi cha pili na kushinda 2-1.

Akizungumza na Nipashe, Nsanzurwimo alisema anakubali kuwa mabao yalifungwa hayakuwa na matatizo isipokuwa faulo iliyotolewa ambayo ilizaa bao la pili kupitia kwa Kagere.

"Sikatai matokeo wala mabao, ila refa hakuwa makini na tatizo lilianzia kwa msaidizi wake namba moja (Michael Mkongwa kutoka Njombe), alishindwa kabisa kwenda na mchezo.

"Yeye aliona kabisa haikuwa faulo lakini akanyoosha kibendera namna hii soka la Tanzania itakuwa kazi kukua, sheria 17 hazikufuatwa kabisa," alisema kocha huyo raia wa Burundi.

Alisema anakubali uwezo mkubwa ulionyeshwa na kikosi cha Simba huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kumiliki mchezo zaidi kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao la kuongoza.

"Simba ina uwezo mkubwa na wachezaji wazuri, lakini niwapongeze wachezaji wangu kwa kumiliki mchezo kipindi cha kwanza katika mechi hii ambayo waamuzi walifanya makosa mengi kinyume cha sheria 17 za soka," alisema.


Katika mechi hiyo, Mbeya City ambayo ilimiliki mpira zaidi kipindi cha kwanza, kama ingeendelea kushambulia mwanzo mwisho, ingeweza kupata mabao zaidi ya mawili, lakini ilipopata bao la kuongoza, ilicheza mchezo wa kujilinda zaidi na kutoa nafasi kwa Simba kuwashambulia

Post a Comment

0 Comments