Windows

Tetesi za usajili Simba 6 May 2019

Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema anataka kuongeza wachezaji wanne tu msimu ujao ikiwa ni mabeki wawili, kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja kwa ajili ya michezo ya klabu bingwa Afrika.
Pia kocha huyo amesema ligi kuu ya Tanzania haina ubora mkubwa kwa sababu timu nyingi ni dhaifu amedai kati ya timu 20 unaweza ukakuta timu 5 tu ambazo zina ubora wa kushindana sawa ila zingine ni dhaifu kwa ubora wa ligi kuu, ndio maana wanashinda kwa urahisi licha ya ratiba ngumu kwao.
Simba mpaka sasa wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa nyuma kwa points 2 nyuma ya Yanga lakini Simba wakiwa na Faida ya kuwa na mechi 4 za ziada.
The post Tetesi za usajili Simba 6 May 2019 appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.


Post a Comment

0 Comments