Windows

MASHINE NNE MPYA KUTUA SIMBA


Imeripotiwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema anataka kuongeza wachezaji wanne tu msimu ujao.

Aussems ameyasema hayo baada ya mchezo wa jana katika Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons kumalizika huku wakishinda kwa mabo 1-0.

Kocha huyo amesema ana malengo hayo ya kusajili ikiwa ni pamoja na beki wawili kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja kwa ajili ya michezo ya klabu bingwa Afrika.

Aidha kocha huyo amesema ligi kuu ya Tanzania haina ubora mkubwa kwa sababu timu nyingi ni dhaifu.

Aussems amedai kati ya timu 20 unaweza ukakuta timu 5 tu ambazo zina ubora wa kushindana sawa ila zingine ni dhaifu ndio maana wanashinda kwa urahisi hali inayowapelekea kupata changamoto kubwa wanapotoka nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments