LEO Yanga ataikaribisha Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00.
Mchezo wao wa kwanza waliocheza uwanja wa Sokoine, Yanga ilibeba pointi tatu kwa kushinda mabao 3-1.
Mechi zao za mwisho za ligi kabla ya leo kumenyana matokeo yao yalikuwa namna hii:-
Yanga ilitoka sare na Ndanda FC uwanja wa Nagwanda kwa kufungana bao 1-1, Yanga 2-0 African Lyon, uwanja wa CCM Kirumba, Yanga 3-2 Kagera Sugar, uwanja wa CCM Kirumba, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga, uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Yanga 1-0 Azam, uwanja wa Uhuru.
Katika michezo mitano Yanga imeshinda mitatu imetoa sare moja na kupoteza mchezo mmoja, ina jumla ya mabao matano ya kufunga na imefungwa mabao manne.
Prisons wao michezo yao mitano walifungwa mabao 2-1 na Singida United, Namfua, walishinda mbele ya African Lyon 1-2 uwanja wa Uhuru, walishinda mbele ya JKT Tanzania 2-0 uwanja wa Isamuhyo, walishinda mbele ya Mwadui 2-0 uwanja wa Sokoine na suluhu mbele ya Biashara United uwanja wa Sokoine.
Katika michezo mitano, Prisons imeshinda michezo mitatu, wamepoteza mchezo mmoja na sare moja, wamefunga jumla ya mabao saba na kufungwa jumla ya mabao matatu.
0 Comments