Windows

VIDEO: Wanachama 1341 kupiga kura ya kumpata mrithi wa Manji Yanga

Mwanaspoti, Michezo, Michezo blog, Wanachama 1341, kupiga kura, uchaguzi, wa Yanga, Mwanasport, MICHEZO

Wagombea watano wanachuana kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti na wagombea 22 wanawania ujumbe huku wanane pekee ndiyo wakihitajika kwenye nafasi hiyo.
Awali Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amesema Yanga ni klabu kubwa inapashwa kuwa na uongozi bora na ushikamano
Alisema tangu ameingia katika wizara hiyo anamiaka miwili ameshuhudia magumu wanayopitia anaomba wayamalize kwa kuhakikisha wanachagua viongozi makini ambao watatatua matatizo.
"Kuna wanachama hawaitakii mema Yanga wamekuwa wakikimbilia mahakamani sio jambo jema ni kudidimiza soka hivyo ni muda wa kuacha mambo kama hayo kwa manufaa klabu."
"Yanga ina watu wengi ndani na nje ya nchi ni muda wa kuifanya Yanga iachane na tabia ya kutegemea mtu wanatakiwa kujiendesha wenyewe hivyo ni muda wa kutafuta viongozi wenye upeo wa kuwapa mabadiliko,"
"Yanga leo inatakiwa kuandika historia ya kuchagua viongozi bora ambao watakuwa na maono ya kuhakikisha wanaingia kwenye mfumo wa kisasa wa kiuendeshaji,"
Naye Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewaomba viongozi watakaopata nafasi ya kuiongoza klabu hiyo wapambane kuhakikisha wanairudisha katika mstari.
Uongozi sio lele mama sio kula bata au umaarufu uongozi ni mzigo na ni kazi ngumu na ndio maana wanasema mzigo mpe mnyamwezi.
"Wanachama mnatakiwa kutulia kuchagua viongozi imara na watakaokuwa na umoja na ushirikoano wa kutosha ili kuwadhihirishia watani wao Simba kwamba kihama chao kimefika,"


Post a Comment

0 Comments