Windows

Vidal anasa kwa kimwana mtunisha misuli



NYOTA wa Barcelona, Arturo Vidal, amenasa kwa kimwana mtunisha misuli raia wa Colombia, Sonia Isaza, wakionekana kuponda raha katika fukwe za kifahari nchini Marekani.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kimwana huyo alitupia picha juzi kwenye mtandao wake wa kijamii wa Istagram akiwa na nyota huyo wakiwa wanaota jua katika ufukwe mmoja uliopo California.

Vidal alishawahi kutangaza kutengana na mkewe, Maria Teresa Matus, ambaye ameishi naye kwa muda wa miaka minne, na sasa amehamisha mahaba yake kwa mlimbwende huyo mwenye umri wa miaka 35, mama wa watoto wawili.

Isaza, ambaye ni mzaliwa wa mji wa Pereira nchini Colombia, alihamia nchini Marekani mwaka 2006, ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa mtunisha misuli mwenye ushindani.

Post a Comment

0 Comments