


Liverpool, England. Beki, Virgil van Dijk anakuna kichwa kutafakari baada ya kuwapo madai kwamba amesema Lionel Messi si mchezaji mzuri kabisa kukabiliana naye.
Beki huyo Mdachi alikabiliana na Messi kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo fowadi huyo wa Kiargentina alifunga mara mbili kuisaidia Barcelona kushinda 3-0 dhidi ya Liverpool uwanjani Nou Camp.
Na sasa wakati mechi ya marudiano ikitarajia kufanyika kesho Jumanne, Van Dijk alidaiwa kumzungumzia Messi akisema kwamba mchezaji huyo hakabiki.
“Anapokuwa kwenye ubora wake, hakuna unachoweza kukifanya kumzuia,: alisema Van Dijk kama ilivyodaiwa.
“Nafurahi sichezi Hispania kwamba ningekuwa nakabiliana naye kila msimu.”
Lakini, Van Dijk amedai kwamba hakuwahi kusema maneno kama hayo na kusema hicho kilichosemwa uongo mkubwa. Jambo hilo linadaiwa kumvuruga sana mchezaji huyo, ambaye bila ya shaka kocha Jurgen Klopp atamhitaji kuwa kwenye ubora wake hiyo Jumanne ili wafanyikiwe kupindua meza kwenye nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Liverpool ina mlima wa kupindua matokeo ya kichapo cha Bao Tatu Bila ili kutinga fainali ya michuano hiyo.



0 Comments