Windows

Manchester United yatangaza dau Pogba kwa Real Madrid

Mwanaspoti, Michezo, Michezo blog, Manchester United, yatangaza, dau Pogba, kwa Real Madrid, Mwanasport

Madrid, Hispania. Real Madrid inaamini kuwa ina nafasi kubwa ya kumnasa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba lakini dau lililowekwa na klabu yake kumuuza nyota huyo linawapa wasiwasi kumpata.


Maisha ya Pogba ndani ya Manchester United yanaonekana kuelekea ukingoni kutokana na kile kinachotajwa tabia zake zilizokithiri za utovu wa nidhamu na inasemekana kuwa klabu hiyo ipo tayari kupokea ofa kutoka klabu nyingine ili imuachie kiungo huyo wa Ufaransa.


Real Madrid inaonekana ndio timu yenye nafasi kubwa kutokana na mahaba ambayo kocha wake Zinedine Zidane anayo kwa nyota huyo ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu aliyoipata baada ya Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia mwaka jana.


Lakini pamoja na Real Madrid kutaka kutumia ushawishi wa Zidane ili kumnasa kiungo huyo wakati wa usajili wa majira ya kiangazi, timu hiyo ya Hispania inadaiwa kuwa haiko tayari kutoa kitita cha Pauni 150 milioni (zaidi ya Sh454 milioni) ambazo Manchester United inahitaji ili kumuachia kiungo huyo.


Wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola inasadikika ameanza kutumia mbinu za ushawishi kwa Manchester United ili ikubali kumuuza kwa dau la chini pungufu ya hilo wanalohitaji lakini klabu hiyo inadaiwa kuwa imeshikilia msimamo wake kuwa Pogba hawezi kuuzwa chini ya Pauni 150 milioni.


Baada ya kuwa na msimu usiovutia, ikikosa mataji yote makubwa ambayo ni lile la Mabingwa Ulaya pamoja na Kombe la Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid inaonekana kujipanga vilivyo kurudisha heshima yake msimu ujao kwa kufanya usajili wa baadhi ya nyota wakubwa ili kuimarisha kikosi chake.


Pogba anaendelea kuwa pendekezo la kwanza la kocha Zidane pia timu hiyo inaonekana kumtolea jicho vilivyo kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard.


Post a Comment

0 Comments