


KOCHA Maurizio Sarri amelazimika kuikosa safari ya Chelsea kwenda kutembelea jumba la makumbusho la Holocaust Memorial lililopo nchini Marekani, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa tumbo.
Sarri alikutana na hali hiyo wakati timu yake hiyo ya Chelsea ikianza ziara ya kujiandaa na msimu ujao, ambapo mapema wiki hii walikipiga na New England Revolution katika mchezo wa krafiki.
Hata hivyo, wakati kikosi cha wachezaji 23 pamoja na jopo la wafanyakazi na mwenyekiti wa, Bruce Buck wakisafiri kwenda Marekani, ndipo ilipofahamika Sarri hakuwapo.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, Sarri alikumbwa na matatizo ya tumbo na hivyo akaamriwa na madaktari abaki katika hoteli ya timu yake hiyo.



0 Comments