Windows

Ubingwa Simba wapelekwa Morogoro, mashabiki Dar wanuna

Mwanaspoti, Ubingwa, Simba, wapelekwa, Morogoro, mashabiki Dar wanuna Kukosekana kwa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kumetajwa ndiyo sababu ya Simba kutokabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara na sasa itafanyika hivyo Jumanne kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Leo Jumamosi, Simba walipaswa kukabidhiwa kombe katika mchezo wake wake dhidi ya Biashara United uliomalizika kwa sare 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.


Wakati mechi hiyo iliyoshudiwa na mashabiki wachecha kwenye Uwanja wa Taifa ikiendelea klabu ya Simba ilitoa taarifa kuwa ubingwa usingekabidhiwa kutokana na mvua, lakini mwisho bodi ya ligi ilisema ni kutokana kutokuwepo kwa mgeni wa heshima.


Mkurungezi wa bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema walishindwa kukabidhi kombe hilo kutokana mgeni ramsi Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kupata dharura.


Wambura alisema; "Kila kitu kitakamilika mjini Morogoro ambapo itakuwa ndiyo mechi ya mwisho ya Ligi Kuu, tumeshindwa kukabidhi kombe kwasababu mgeni ramsi hajafika, amepatwa na dharura. Tunaipongeza Simba kutwaa ubingwa, ligi ilikuwa ndefu kwasababu timu zipo nyingi.


"Tulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo mabadiliko ya ratiba yaliyotokana na mechi za CAF pamoja na kukosa udhamini, hivyo msimu ujao tutajipanga kuona mambo yanakwenda vizuri," alisema Wambura

Post a Comment

0 Comments