

Kesho Jumanne, May 28 2019 ligi kuu ya Tanzania Bara inafikia tamati kwa Yanga kushuka katika dimba la Uhuru kuikabili Azam Fc
Yanga imejihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili ambapo itapata zawadi ya Tsh Milioni 40 wakati mabingwa Simba wakipata Mil 80
Licha ya kumaliza msimu bila taji lolote, wachezaji wa Yanga wanastahili pongezi, kwani walijitoa kwelikweli bila ya kujali mazingira magumu yaliyokuwa yakiwakabili
Uongozi wa Yanga umejifunza jambo msimu huu na wamechukua hatua kuhakikisha matatizo yaliyotokea hayajirudii
Hatua ya dharura iliyochukuliwa na uongozi kwa kushirikiana na kocha Mwinyi Zahera, kuendesha zoezi la kuichangia Yanga, inaelekea kuiwezesha timu hiyo kufanya usajili mkubwa hali ambayo imeanza kuwatishia wapinzani wao Simba
Yanga imepanga kutumia kati ya Bil 1.5 na Bil 2 kwa ajili ya usajili msimu huu huku ikitenga kiasi kingine kwa ajili ya mishahara ya wachezaji kwa angalau msimu mmoja
Fedha hizo zinapatikana kupitia michango ya wadau wa klabu hiyo, zoezi lililoendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ambalo litafika tamati Juni 15 kwa tukio kubwa la Harambee kufanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Tayari idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni wako nchini kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria
Wakati wengine wakija kusaini mikataba, baadhi wanakuja kufanya majaribio kulishawishi benchi la ufundi
Wiki iliyopita, kocha Zahera alisema ataongeza wachezaji wa kigeni saba katika kikosi chake huku akibainisha kusajili wachezaji wazawa wannecut
Baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, Yanga itaweka hadharani majina ya wachezaji ambao tayari wamesajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ambapo imeelezwa wachezaji nane(sita wa kigeni na wazawa wawili) wako kwenye hatua za mwisho kusajiliwa
Aidha idadi na majina ya wachezaji wanaoachwa na Yanga pia watafahamika baada ya mchezo dhidi ya Azam
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewahakikishia wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao kwani wamepania kurudisha hadhi ya timu hiyo
"Msimu ujao tumedhamiria kuwa na timu imara, tutashirikiana na benchi la ufundi kuwawezesha kila watakachohitaji kuhakikisha tunatengeneza timu ya ushindani"



0 Comments