Windows

Kocha Mbeya City kusuka upya kikosi

KOCHA Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo, amepanga kusuka upya kikosi chake kama atafanikiwa kubaki kwenye timu hiyo.
Akizungumza na BINGWA jana, Nsanzurwimo, alisema mkataba wake na Mbeya City umemalizika lakini yuko tayari kuongeza mwingine akiwa na lengo la kuifufua timu kama ilivyokuwa zamani.
Alisema kipindi anajiunga na timu hiyo alikuwa anahitaji kuweka rekodi ya pekee na kutengeneza kikosi cha ushindani kama ilivyokuwa msimu wao wa kwanza wakati inapanda daraja.
Nsanzurwimo alisema alikuwa anaifahamu Mbeya City kuwa ni timu tishio Ligi Kuu Tanzania Bara, pia ina mashabiki wengi lakini kwa misimu miwili mfululizo haijafanya vizuri.
“Nilivyokabidhiwa Mbeya City nilikuwa  nataka kutengeneza rekodi ya tofauti, yaani kuirudisha timu katika enzi zake, lakini kutokana na changamoto mbalimbali imeshindikana,” alisema kocha huyo.
“Msimu huu umekwisha na tunamaliza katika nafasi ambayo sijaipenda, licha ya kwamba mkataba wangu unaisha nipo tayari kuongeza ili kutengeneza Mbeya City mpya msimu ujao,” aliongeza.
Kwasasa Mbeya City ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 47, alizokusanya  kutokana na mechi 37, wakishinda 13 wakitoka sare nane na kupoteza 16.

Post a Comment

0 Comments