

Msemaji wa Yanga Dismas Ten ameipongeza AzamTv kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia matarajio ya wengi katika urushwaji wa mechi za ligi kuu
Ten amesema baada ya ligi kumalizika na bingwa kupatikana, ni wakati wa kufanya tathmini ili kuboresha zaidi msimu ujao
"Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana AzamTV hakika mmefanya kazi kubwa na ya kiwango cha juu," ameandika Ten katika ukurasa wake wa Instagram
"Mechi na matukio mengi mmerusha live bila chenga wala mikwaruzo"
"Kupitia ninyi tumeona soka safi kwa mechi za mikoani pia Dar es Salaam, vituko na hata matukio yasiyo ya kawaida yakiwemo yale yaliyoibua mijadala mikubwa miongoni mwa wapenda soka, matukio kama Penalti, offsides, fouls zenye utata"
"Kwenye kila jambo changamoto hazikosi ni vyema kuangalia palipo na mapungufu ili msimu ujao mfanye vizuri zaidi"
Azam TV itaendelea kurusha matangazo ya ligi kuu msimu ujao kwani miaka miwili iliyopita, walisaini mkataba wa miaka mitano na TFF



0 Comments