Windows

Simba waonywa kwa Wawa



KOCHA Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18, Abdallah Mohamed ‘Bares’, amesema beki wa Simba, Pascal Wawa, hastahili kuendelea kuitumikia timu hiyo na badala yake uongozi unatakiwa kutafuta mlinzi bora zaidi yake.

Akizungumza na BINGWA juzi, Bares ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha JKT Tanzania, alisema Simba inatakiwa kufanya usajili kulingana na hadhi ya mashindano ya kimataifa watakayoshiriki mwakani.

“Binafsi kwa msimu ujao sioni kama Wawa anastahili kuendelea kuwapo Simba, kwani licha ya uzoefu wa kimataifa alionao lakini bado ana mapungufu mengi ambayo hayapaswi kuonekana katika kikosi hicho mwakani,” alisema kocha huyo.

“Ushauri wangu kwa benchi la ufundi la Simba na viongozi kwa ujumla watakapotaka kufanya usajili waanze na beki ambaye Wawa anacheza kisha wakaongeze nguvu mbele, kwani Emmanuel Okwi naye ameonekana kuchoka hivyo anahitaji wa kumsaidia.”

Post a Comment

0 Comments