

Tanzania Prisons 0-1 Simba
Uwanja: Sokoine
Okwi goal dk ya 11
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi leo ameandika bao lake la 11 kwenye mchezo kati ya Tanzania Prisons na Simba unaochezwa Uwanja wa Sokoine.
Okwi amefunga bao hilo dakika ya 11 akimalizia pasi ya James Kotei baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Prisons kabla ya kuzamisha mpira kwenye nyavu.
Huu ni mchezo wa pili Simba kucheza uwanja wa Sokoine baada ya juzi kucheza dhidi ya Mbeya City.
Simba wanakumbukumbu ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, Tanzania Prisons wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, uwanja wa Uhuru.




0 Comments