LIVERPOOL itakabiliana na Tottenham Hotspur kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Juni 1, mwaka huu katika Uwanja wa Metropolitano mjini Madrid, Hispania.
Fainali hiyo itapigwa saa 4.00 usiku kwa saa za Tanzania katika Uwanja wa Wanda Metropolitano unaomilikiwa na klabu ya Atletico Madrid ya Hispania.
Liverpool ndio ilitangulia fainali baada ya kuicharaza Barcelona mabao 4-0 juzi kwenye Uwanja wa Anfi eld na kupindua matokeo kwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kulizwa mabao 3-0 ugenini kwenye Uwanja wa Nou Camp, wiki iliyopita.
Hakuna aliyetegemea Liverpool ingeibuka na ushindi huo wa kihistoria kutokana na kuteswa na Barcelona na hasa nyota wao, Lionel Messi kwenye mchezo wa kwanza.
Hata hivyo, mabao mawili ya Divock Origi na mengine ya Georginio Wijnaldum yaliisaidia Liverpool kuzima ndoto za Barcelona za kutwaa taji la ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2018/19.
Liverpool iliyowahi kutwaa taji SPURS hilo mara tano, imetinga fainali kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kulizwa na Real Madrid mabao 3-1 katika msimu wa 2017/18 kwenye fainali.
Tottenham Hotspur nayo ilifuata nyayo za Liverpool kwa kufanya maajabu ya kupindua matokeo baada ya kuiliza Ajax Amsterdam mabao 3-2 kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali jana kwenye uwanja wao wa Johan Cruyff.
Kumbuka Tottenham ililala bao 1-0 nyumbani kwa Ajax kwenye mechi ya kwanza lakini kwa ushindi huo imesonga mbele kwa sheria ya goli la ugenini baada ya timu hizo kuwa zimefungana jumla ya mabao 3-3. Shujaa kwa Tottenham alikuwa mbrazili Lucas Moura, ambaye alipiga `hat-trick’ (mabao matatu katika mechi) kwenye mchezo huo.
Ajax ilianza kwa kasi mchezo wa jana na kujipatia bao mapema dakika ya tano lililofungwa kwa kichwa na nahodha Matthijs de Ligt baada ya kuunganisha mpira wa kona.
Hakima Ziyech aliongeza bao la pili la Ajax katika dakika ya 36 kufuatia kazi nzuri ya Dusan Tadic kumpokonya mpira Kieran Trippier na kuingia na mpira kwenye eneo la Tottenham kabla ya kutoa pasi safi kwa mfungaji aliyepiga shuti kali lililotinga wavuni.
Lucas Moura alipachika bao la kwanza la Tottenham katika dakika ya 55 kufuatia pasi ya Dele Alli. Dakika tano baadae Moura aliisawazishia Tottenham baada ya kuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Ajax, Andre Onana na kuujaza mpira wavuni kwa shuti la chini.
Moura aliipeleka fainali Tottenham baada ya kuujaza mpira wavuni katika dakika ya 96 baada ya kupokea pasi ya kubetua ya Alli.
Liverpool itakaipovaa Tottenham itakuwa inawania kutwaa taji hilo kwa mara ya sita kufuatia mafanikio ya kulibeba miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005. Tottenham kwa upande wao imeandika historia kwa kufi ka fainali kwa mara ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
The post Tottenham Yaishangaza Ajax, Yatinga Fainali Uefa (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.
0 Comments