MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe, amempongeza straika wa Simba, Meddie Kagere, kwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2018/19.
Tambwe amewahi kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa misimu miwili tofauti, 2013/14, akifunga mabao 19, wakati akiwa Simba na Yanga msimu wa 2015/16 akiibuka kinara kwa kufunga mabao 21.
Kagere amekuwa mfungaji bora msimu uliomalizika hivi karibuni kwa kufunga mabao 23 na kufanikisha timu yake kutwaa ubingwa.
Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema mwenendo wa Kagere tangu alipoanza kuchezea Simba, alionyesha matumaini ya kuvunja rekodi yake kutokana na kasi yake ya kufunga.
“Nampongeza Kagere kwa uwezo alioonyesha na kufanikiwa kuibuka mfungaji bora, kwa juhudi yake kama ataendelea kuwepo atakuja kuwa mfungaji hata mara mbili.
“Ni mchezaji niliyemuona na kipaji cha pekee, kazi anayofanya ndicho anachotakiwa kufanya straika yeyote,” alisema Tambwe.
0 Comments