

Baada ya kufungwa mabao 2-0 na JKT Tanzania leo, Stand United imeungana na African Lyon kuteremka daraja
Kagera Sugar imeponea chupuchupu kushuka moja kwa moja ikitofautiana mabao na Stand United zote zikiwa na alama 44 lakini sasa imeungana na Mwadui Fc kucheza mtoano na timu mbili za ligi daraja la kwanza, Pamba Fc na Geita Gold kusaka nafasi ya kubaki ligi kuu/kushuka
Kagera Sugar imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbao FC
Ruvu Shooting imenusurika na kikombe cha kushuka daraja baada ya kuichapa Alliance bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mabatini



0 Comments