Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' juzi alisababisha 'majanga' baada ya kujifunga bao pekee lililoihakishia Kagera Sugar ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Simba
Tshabalala alichanganyana na mlinda lango Aishi Manula hali iliyopelekea wote watokee majaro iliyokuwa imechongwa kutoka wingi ya kushoto tukio lilisababisha Tshabalala aujaze mpira kimiani
Baada ya tukio hilo, Manula alimvaa Tshabalala na wawili hao 'kushikana mashati' kabla Mlipili hajaingilia kati kumuondoa Tshabalala eneo la tukio
Manula amesema tukio lililotokea uwanjani kati yao lilisababishwa na presha ya mchezo lakini liliishia palepale uwanjani, hawana tatizo nje ya uwanja
"Hatukuwa na mawasiliano mazuri," amesema Manula ambaye pia ni mlinda lango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania
"Kilichotokea pale kilisababishwa na presha ya mchezo tu, Tshabalala ni rafiki yangu na tumekuwa tukishirikiana katika masuala mbalimbali"
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alilizungumzia tukio hilo ambapo alisema limechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchovu wa wachezaji wake ambao wamekuwa wakicheza mfululizo
"Tumecheza michezo saba ndani ya siku 16, wachezaji wangu ni binadamu, wanachoka. Ndio maana baadhi ya matukio wanayofanya yanasameheka kwa kuwa najua yanasababishwa na mazingira yanayotukabili"

0 Comments