KOCHA wa kikosi cha Timu ya Biashara United, Amri Said amesema kuwa hesabu kubwa za kikosi lazima zitimie kwa kubaki kwenye ligi msimu ujao.
Biashara United imepanda daraja msimu huu na imekuwa na matokeo ya kusuasua kwani katika michezo 34 ambayo imecheza imeshinda michezo 10 na kupoteza michezo 14 na imetoa sare michezo 10 ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 40.
Said alilipa kisasi cha kufungwa mabao 2-1 na Yanga uwanja wa Taifa kwenye mchezo wao uliochezwa uwanja wa Karume, Mara kwa kushinda bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa kikubwa ambacho kilikuwa kinaimaliza timu yake ni ubutu wa safu ya ushambuliaji pamoja na uwezo wa kujiamini hasa wanapoingia kwenye eneo la hatari.
"Haikuwa kazi nyepesi kupata matokeo ila niligundua kilichokuwa kinaiponza timu yangu ni uwezo wa kujiamini na ubutu wa safu ya ushambuliaji, kwa sasa bado nina nafasi ya kupata matokeo kwenye michezo yangu minne iliyobaki," amesema Said.
0 Comments