Windows

Simba yajiapiza kuichapa Prisons mapema tu Sokoine

Mwanasport, Mwanaspoti, Simba, yajiapiza, kuichaka, Prisons, Michezo, Michezo blog, uwanja Sokoine, MICHEZO
Mbeya. Simba leo Jumapili itaingia uwanjani ikiwa ni siku moja kutoka kucheza na Mbeya City, ambapo sasa wana kibarua dhidi ya Tanzania Prisons.
Timu hizo zote zinahitaji ushindi, ambapo Simba inapambana kutetea ubingwa wake na kujiweka pazuri kwenye msimamo, ambapo kwa sasa iko nafasi ya pili ikiwa na alama 75 huku watani wao Yanga wanaoongoza wakiwa na alama 80.
Hii itakuwa mechi ya 30 kwa Simba ikibakiza mechi tisa kumaliza ligi wakati Yanga wao wamebakiza mechi nne huku Prisons wanaoshika nafasi ya tisa wakicheza mechi 33 zikibaki sita na wana pointi 42.
Prisons ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, wataingia wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Yanga pale Uhuru, Dar es Salaam, kwa mabao 2-1.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Taifa, Prisons walipigwa bao 1-0, shukrani kwa Meddie Kagere aliyefikisha mabao 17 sasa.
Beki wa Simba, Erasto Nyoni aliliambia Mwanapsoti kuwa, wamejipanga kwa mchezo huo kwani lengo ni kuondoka na pointi sita jijini hapa.
Alisema licha ya uwanja kujaa maji na tope kutokana na mvua inayoendelea, watapambana ingawa hawatacheza soka la kuvutia.
“Tunajua hii ni hali ambayo hatuwezi kuikwepa, tunachosema ni kuwa, tutakomaa kupata matokeo mazuri,” alisema Nyoni.
PRISONS HAWANA PRESHA
Wakati Simba wakionekana kuwa na presha na mechi hiyo kutokana na malengo ya kutetea ubingwa, huko Prisons wanatambua kuwa ni mechi ngumu ila wanaamini watashinda tu.
Kocha wa timu hiyo, Adolf Rishard alisema anatambua ugumu wa mechi hiyo lakini amewatoa hofu wachezaji wake kutocheza kwa presha ambako kunaweza kuwasababisha wapoteze mchezo.
Alisema wanafahamu kiwango cha wapinzani wao lakini vijana wapo vizuri na wana shauku kubwa kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ligi hiyo.
"Tunataka kuleta heshima uwanja wa nyumbani, hatuwahofii Simba, tumewoana wakicheza na Mbeya City, tutayatumia mapungufu yao kushinda,'’ alisema Rishard.
MAJERUHI SIMBA WAONGEZEKA
Beki Paul Bukaba juzi alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya kuumia goti, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Nyoni. Taarifa ni kwamba, Bukaba atakuwa nje hadi mwishoni mwa msimu.
Nyota wengine waliokuwa majeruhi ni Shomary Kpaombe, Paschal Wawa, John Bocco na Asante Kwasi ingawa imeelezwa kuwa, wataanza mazoezi na timu hiyo mara itakaporejea kutoka Mbeya ikijiandaa na mechi dhidi ya Coastal Union.

Post a Comment

0 Comments