Windows

Simba washinda kwa JKT bao la jioni

Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Simba kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania leo, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.

Simba imepata ushindi huo kunako dakika ya 90 zikiwa zimeongezwa 7 kupitia kwa Hassan Dilunga aliyeingia kipindi cha kwanza akichukua nafasi ya John Bocco.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 72 wakibaki nafasi ya pili huku Yanga akiwa bado kileleni na pointi zake 77. Lakini pia Simba inahitaji alama 21 kwenye mechi 10 zilizo salia kutangazwa mabingwa wa TPL.

Juhudi kubwa za mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyewavuruga mabeki wa JKT kwa chenga kabla ya kumpenyezea mpira mfungaji.

Vikosi vya timu zote mbili vilikuwa hivi:

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Zana Coulibaly/Nicholas Gyan dk70, Mohammed Hussein, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/Rashid Juma dk59, Clatous Chama, Muzamil Yassin, John Bocco/Hassan Dilunga dk30, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.

JKT Tanzania; Abdulrahman Mohammed, Anuary Kilemile, Salim Aziz Gilla/Saad Abubakar dk80, Rahim Juma, Frank Nchimbi, Nurdin Mohamed, Najim Magulu, Mwinyi Kazimoto, Samuel Kamuntu, Edward Songo na Richard Maranya/Kelvin Nashon dk87.


Post a Comment

0 Comments