Windows

Serikali kujenga kituo cha taarifa msitu wa Nyumbani Njombe


Na. Amiri kilagalila, Njombe

Ili kuendelea kukuza sekta na vivutio vya utalii mkoani Njombe na nchi kwa ujumla,naibu waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezo Juliana Shonza amemuagiza mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe kujenga kituo maalumu cha kutoa taarifa katika msitu wa nyumbani tu wilayani humo uliokuwa ukitumiwa na makabila 91 nchini kwa ajili ya Ibada za jadi.

Naibu waziri ametoa agizo hilo alipotembelea msitu huo wa asili unaowavutia watu wengi wa mkoa wa Njombe na mikoa ya jirani kufika katika eneo hilo kujifunza kutokana na historia yake pamoja na uwepo wa kuku weusi wanaopatikana ndani ya msitu huo.

“Maeneo haya ni muhimu sana na  nimeambiwa idadi ya wanaokuja hapa kutembelea ni 30 kwa mwaka hii idadi ni ndogo sana kwa hiyo bado kuna kazi haijafanyika kwa hatua za wilaya na hata mkoa,na maeneo haya ni muhimu sana yalishatumika kwenye mapigano wakati wakupigania uhuru,kwa hiyo niombe tu utekelezaji uanze hata wa kujenga kituo cha kutolea taarifa hapa ili zipatikane kwa urahisi”alisema Shonza

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally  kasinge amebainisha mkakati juu ya kivutio hicho katika wilaya yake ikiwemo kuweka utaratibu wa kituo cha taarifa cha wilaya.

“Mikakati ambayo sisi kama wilaya tumekuwa nayo ni pamoja na kukusudia kuwa na kituo cha taarifa cha wilaya ili haya yote wanayo yaeleza wazee hawa yapatikane katika maandishi lakini katika makala zingine ikiwemo za video”amesema Kasinge

Chief wa kabila la wabena mzee Elias Mkongwa akitoa historia fupi ya msitu huo amesema msitu huo unaombatana na mapango ulikuwa ukitumika na makabila 91 nchini katika kufanya ibada huku mapango yakitumika kujificha katika vita vya makabila.

Aidha Waziri Shonza ametembelea jiwe lenye ukubwa wa ekari 7.5 lililopo kijiji cha Igodivaa kata ya Imalinyi wilayani humo huku likiwa na picha ya ramani ya Afrika juu yake pamoja na miti yenye maua isiyo kauka vipindi vyote na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa ajili ya utalii katika maeneo hayo kwa kuwa mpango wa serikali kwa sasa ni kuviendeleza vivutio hivyo.


Post a Comment

0 Comments